Kesho sio ajali,Kesho ni Leo iliyoandaliwa,Matumaini makubwa ya kesho, maandalizi yake ni leo.Ukitaka kujua utakua vipi kesho angalia tuu tabia zako,unafanya nini kuanzia unamka hadi unaenda kulala,ndio maana hata hapo ofisini kuna wanaolia uchumi mbovu na kuna wanaonawiri maana mbegu walipanda machozi yao ni matone yanayoisaidia hiyo mbegu kuota.
Unachokifanya Leo ni mbegu utavuna.. Hayo maono ni mbegu usiyale yafukie mchangani,utavuna...... Wengi wamekula mbegu zao wanapowaona wengine wanakula mavuno yao,usikule mbegu... Anafanya jambo jipya je hatukuliona? Macho yanashuhudia Masikio kusikia.. Heri siku Moja mbele zako kuliko siku elfu mbali na wewe. Heri nikose vyote na nikupate wewe......
Soma nami Isaiah 43:1-5
1.Lakini sasa, Bwana aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
2.Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.
3 Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.
4 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.
5 Usiogope; maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi;
6 nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.
SHUKRANI MUHIMU
Midomo isiyo na shukrani hukausha mema yote Mshukuru Mungu hata kwa hicho kidogo ulichonacho wakati unasubiria makubwa kutoka kwa Mungu. Mungu akupe moyo wa shukrani kwani midomo isiyo na Shukrani inakausha mema yote.
No Comments Yet...