Wanafunzi wa kozi zote za Uhandisi walikutana kwenye ukumbi mkubwa. Kilichowakutanisha hakikuwa michezo wala soga. Ni lile somo pendwa la wahandisi, yaani ENGINEERING MATHEMATICS. Hili lilikuwa somo la lazima kwetu. Wale wa Mechanical Engineering, Civil na sisi wa kozi ya Umeme na Electroniki, tulikutana darasani kunolewa, kwenye kipindi maarufu cha hesabu. Ni mwaka wa kwanza Chuo kikuu.
Lecturer walipoingia darasani na notes chache. Mwanafunzi mmoja alimpenda tangu mwanzo. Hakuwa na makuu yule baba wa watu. Anaongea kwa sauti. Anasikika vema. Shati lake la mikono mifupi na miwani yake, vilimfanya aonekane nadhifu haswa. Baada ya kusalimiana na wanafunzi, zilifuata dakika chache za utambulisho na hasa kufahamiana kwa majina. Utambulisho ukaisha mapema.
Bila kupoteza muda akaanza kufundisha na kuandika notes. Wanafunzi wote ni wapya, wenye ndoto ya kuwa mainjinia miaka Minne baadaye. Ndo yameanza rasmi Na kwa kuwa wanafunzi wengi wanajua hakunaga tuition za masomo ya Pre-University, walikuwa na uhakika kwamba wote pale ni wageni na topic ile.
Yule mwalimu hakuwa na utani na kufundisha hesabu. Alikuwa na bidii kama anafanya huduma. Na ukweli usemwe, anajua hesabu. Ubao ulizidi kuchafuka, ni formula baada ya formula. Kila mstari ni formula mpya.
Darasa lilikuwa limetulia tuli. Somo likaendelea. Notes waandika. Hapo bado kama dakika 10 muda wa kipindi uishe, lakini mwanafunzi mmoja kuna kitu akilini mwangu hakikuwa sawa. Yaani alikuwepo kimwili darasani, lakini akili yake haikuwepo.
Alisikika akimwelezea mwanafunzi mwenzake ,Nikwambie ukweli? Siku ile sikuelewa kitu. Maana yake nini mambo haya? Nilijisemea Najiuliza maswali mengi sana. Hii hesabu mbona kama naona nimeshafeli kipindi cha kwanza? Hivi ni kweli mimi ni mjinga kiasi hiki? Dakika 80 zinaisha ila nimeshindwa kuelewa hata formula moja tu jamani?
Nilijilaumu. Nikajichukia. Nikajiona bure kabisa. Kwani nilijiunga na kozi ya Engineering kwa bahati mbaya? Mambo gani haya ya kuaibika ukubwani? Niliwaza si utani Nikiwa kwenye hayo mawazo, mwalimu akahitimisha kipindi. Wengi wetu Tukatoka kimya kama aliyetoka altareni kushiriki mwili na damu ya Bwana. Mimi huyoooooo!!!! Moja kwa moja hadi kwenye kantini ya chuo. Mhudumu!!!! Lete soda. Nikajipatia soda moja teule.
Fundo moja na la pili, taratibu naimeza kupoteza mawazo ya Engineering mathematics. Kamoyo kanapwita. Sijatulia hata hivyo. Bado Naona zile formula zilivyokuwa zinapangana ubaoni. Na mpaka hapo ujue zilishanitoa rohoni kabisa. Hapo katini nipo akatafakari mithali za zamani. Kwamba haya ndo yale ya muuza nyama buchani anakukatia mfupa kwa shoka na anategemea wewe ukautafune kwa meno.
Tupa kule. Nikaondoka kurejea bwenini. Nikawatafuta wenzangu. Nikawauliza vipi jamani, mwalimu wa hesabu anaeleweka? Kila mmoja akasema la kwake. Wengine wanasema anaeleweka. Nikajua hawa wanajifariji tu. Wengi wakasema hapa mambo yameshakuwa magumu. Mimi hapo sijui niondoke na lipi.
Wiki iliyofuata kipindi kikaendelea. Bado mambo yakazidi kunielemea. Bado Sielewi. Naona kabisa kwamba hapa nitafeli.
Anazidi kusimulia labda Yesu anisaidie sana. Tena amtume malaika yule mkuu anisaidie maana naona nimeshazama kama Petro. Mwezi mmoja ulipoisha, mwalimu akatangaza mtihani wa kwanza wa majaribio (test 1).
Niliposikia habari hizi, nikajisemea kama hayati mzee Majuto, KUMEKUCHA.
Siku ya mtihani ikafika. Akawahi na kukaa mbele kabisa. akapewa karatasi ya mtihani. Akasoma. akajisemea moyoni. Huyu mwalimu mbona analeta masikhara kwenye utani. Maswali ni haya haya au kuna mengine?
Amin amin nakwambia, hapakuwa dalili ya kuongezewa karatasi nyingine ya maswali. Akajijibu mwenyewe. Mtihani ndio huu huu. Hapa ni kukomaa. By the way mtihani ule ulikuwa wa ajabu sana. Ilikuwa ni kawaida kukutana na vijiswali viwili tu, hata nusu ukurasa haujafika.
Kama hujajiandaa utaomba na kukemea sana, na utakapofungua macho hutaona malaika. Unasubiriwa wewe uandike. Nisikucoshe. Nilichoandika siku ile, Bwana ajua. Na niseme ukweli, sikufanya vizuri sana.
Matokeo ya Test 1 yakatoka, akapewa haki yangu ya kikatiba. Kwa mara ya kwanza akapata bendera kwenye hesabu Lakini cha kushangaza kwenye ule mtihani kuna wenzake walifanya vizuri sana, hadi mwalimu akawapongeza.
Yeye kusikia kuna mtu kapata A kwenye mtihani ule, aliona wazi hapa yuko Kisiwani Patmo.. na pengine haya ayaonayo ni maono ya mbinguni.. barua kwa makanisa saba.. Wapi bwana. alikuwa darasani kabisa. Akawa anajisemea tu kimya kimya.
Sio kweli kwamba kuna anayeweza kupata A kwa maswali yale. Kapataje? Watakuwa labda wameibia. Haiwezekani labda mtihani ulivuja. Aliondoka pale akiwa amesononeka. Aliumia kiukweli. Akajua hapa analo tatizo. Haraka sana Roho Mtakatifu akaanza kunisemesha, nami nikajiambia, MIMI SIO MJINGA.
SHETANI NIKOME. Pili akajua hapa nahitaji neema ya pekee ya Mungu. Kimbilio lake ni madhabahu. yeye huyo akachukua Biblia yake na notebook. Moja kwa moja pale ghorofani, Block 6, kwenye chumba chao cha sala. Akafika, akaomba. Akalia. Akamsihi Bwana sana sana, kama Mfalme Hezekia. Madhabahu ile ingeulizwa ingemsemea.
Anasema -Nilipokuwa kwenye maombi yale nikasemeshwa jambo. Kwamba tatizo sio ugumu wa masomo. Tatizo ni FIKRA ZANGU. Roho Mtakatifu akanikripia akisema uliona masomo ni magumu na ukachukulia kwamba wote mtafeli. Ulidhani kitakuwa kifo cha wengi harusi. Kumbe wengine walishadhamiria kwamba iwe iwavyo, kufaulu lazima. Nikaambiwa, badili fikra zako. Hilo jambo sio zito kama unavyolichukulia. Kaa na waliofaulu wakupe mbinu. Toka kwenye fikra hasi. Baada ya yale maombi nikatoka. Nikamtafuta rafiki yangu mmoja ambaye alifanya vizuri sana kwenye mtihani ule. Akanipa mbinu. Tukaanza kusoma wote kila siku usiku. Nikaanza kuelewa.
Kumbe inawezekana ee?? Muhula uliofuata na mimi nikaanza kupata A. Tukaendelea hivyo, hadi namaliza mwaka wa nne, A zilishakuwa rafiki zangu wa Karibu. Sio tu kwenye somo la Hesabu, bali hata masomo mengine magumu zaidi. NATAKA KUSEMA NINI KUPITIA STORY HII FUPI? Duniani kuna changamoto nyingi za kiimani na kimaisha. Na watu wengi wakikutana na mambo magumu ya kiroho na kimaisha hudhani wanachowaza wao na wengine wanawaza hicho hicho. Wao Hudhani hakuna atakayetoboa hapa. Hii issue imekaa vibaya. Kwa ile kuamini kwamba HILI HALIWEZEKANI, wanashitukaga sana baadaye wakijua kumbe kuna mtu alifanikiwa pale pale ambapo mimi nilishajua hapawezekani Kafikaje pale? Kapitia wapi? Aaha bana huyu katumia uchawi.
Mungu yuko kwenye biashara kuwainua watu wa utukufu wake, utashanga watu wanasema ,kapataje hela zote hizi kijana mdogo tu? Ni ndumba, sio bure. Ngoja nikwambie kitu. Fikra za aina hii zimechelewesha wengi. Yale mambo unayoyaona magumu kwako, usidhani ni magumu kwa watu wote. Hapa duniani mambo ni mengi lakini muda unatosha, Naam, UNATOSHA KWA WALIOJIANDAA. Yale mambo unayoona yatakuzuia kwenda mbinguni, utashangaa kuna watu ambao watapewa taji na Yesu kwa kuyashinda mambo hayo hayo. Usidhani kwamba hakuna walioshinda dhambi ya ulevi, au ya uzinzi au ya rushwa. Usidhani kwamba kwa sababu wewe unaangamia, basi eti wote wataangamia pamoja na wewe.
Ukiwaza hivyo unapanda upepo, na utavuna tufani. Na usipobadili fikra zako ukaanza kuambatana na wale wenye mawazo ya ushindi, wenye mtazamo chanya kuhusu WOKOVU WA KWELI NA NGUVU HALISI YA MUNGU, Utaangamia mwenyewe. Kabisa. Sikiliza nikwambie. Kuna watu wameingia kwenye majanga kwa sababu waliaminishwa kila mtu anafanya.
Wakaambiwa, unadhani utawezaje wewe kuwa wa kwanza? Na wengi wamejiingiza kwenye majanga wakiamini hivyo ndivyo kila mtu anaishi. Nakuhakikishia. Kuna walioshinda vile vile vinavyokusumbua. Kuna waliopita salama njia ile ile unayoogopa. Kuna waliofanikiwa kiMungu kwenye Biashara hiyo hiyo unayotaka kutumia njia za panya. Kuna waliofanikiwa kuwa marafiki wa Mungu wakiwa na nafasi kubwa kuliko hiyo uliyo nayo kazini.
Tatizo ni kwamba unapokwama na ukashindwa kuvuka unatafuta ushauri kwa wale walioshindwa kama wewe. Waliokwama kama wewe. Nikupe mfano. Unataka kuanza ratiba ya kufunga na kuomba alafu unatafuta ushauri kwa mtu ambaye alisoma Biblia mara ya mwisho zamani za Rais Mwinyi.. Atakushauri nini? Zaidi ya kukukatisha tamaa? Atakwambia ukifunga utakufa Tafuta waliovuka wakuvushe.
Tafuta wasomaji wa Neno wakupe mbinu za kusoma neno. Tafuta waombaji wakupe mbinu za kuomba, katikati ya ubize na mitkasi ya maisha. Tafuta wanaomjua Mungu kibinafsi, wakusaidie namna ya kumjua Mungu. Na sasa unaweza kujua kwa nini hausogei kiroho wala kimaisha, kwa sababu wale wanaokushari wana hali mbaya kuliko yako Kwa sababu unataka ushauri kwa walioshindwa na kukwama kama wewe.
Lini kipofu akachora picha? Tangu lini kobe akamfundisha mbuzi namna ya kupanda juu ya mti? Unataka kuacha pombe lakini unawauliza marafiki zako walevi kama wewe?. Unatarajia msaada gani kwao kuhusu jambo hilo.? Akili yako ina akili? Soma hapa.
Haya ni maneno ya myahudi mmoja, Mwanasayansi Mkongwe aitwaye Albert Einstein. Anasema, PROBLEMS CANNOT BE SOLVED BY THE SAME LEVEL OF THINKING THAT CREATED THEM. Anamaaisha, matatizo hayawezi kutatuliwa na kiwango kile kile cha akili kinacholingana na kile kilichoyatengeneza. Kuna marafiki wenye vitu vingi kukuzidi. Hawa ukiwa nao kuwa makini. Vingi watakavyoongea kama story za kawaida ni shule kwako.
Ukiwa nao ujue uko darasani. Beba vitakusaidia. Kuna marafiki mnaolingana level. Hawa usipoteze muda mwingi nao hata kama mnaelewana. Wanachojua nawe unakijua. Mazungumzo yenu yanapaswa kuwa mafupi. Kwa sababu hakuna jipya. Kuna unaowazidi kiroho. Hawa kuwa makini maana wanakutegemea. If you're not careful they will drain you. Watakunyonya na utaisha. Maana hawakuongezei kitu kipya.
Wanafyonza ulicho nacho. Ni kweli watasaidika lakini kuwa makini. Hata kama wanafurahi na kubarikiwa wakiwa na wewe, jitenge nao sometimes. Nenda tafuta waliokuzidi udake vitu vipya na ukue Ili ukirudi kwa walio chini yako uwe na kitu kipya cha kuwalisha kiakili na kiroho. Mfalme Sulemani aliwahi kusema, "Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia." [Mithali 13:20]
No Comments Yet...