error code:
Sounds FM
Sign-In
Verify Email Address Account Sign-Out
Menu
Homepage News
Program
Schedule Shows Specials
Program
Schedule Shows Specials
Staff

Embed The Radio Player In Your Website
Copy the code below and paste it into your website.

Download our desktop apps

Back to news

Muhubiri 9:11 Si wenye mbio wote washindao katika Michezo.

2025-07-11 07:00:00
9
0

 

Ukiangalia watu wengi wanaofanikiwa katika ulimwengu huu mara nyingi sana husifiwa kwa juhudi, walizonazo pengine hata wao wanapotoa ratiba zao kwa siku zinakuwaje mara nyingi huwa tunaona ni juhudi zao, ustadi wao pengine Elimu zao nk kwa jicho la kawaida unaweza kusema ni kweli na kuna uhalisia ndani yake.

 Lakini sasa tukirudi katika Neno hili alilolizungumza Sulemani kwa hekima aliyopewa na Mungu Kuna jambo la tofauti kidogo hebu tusome..

Mhubiri 9:11 “Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote”. 

Ukisoma kwa makini hapo utaona Sulemani anaanza na kusema “Nikarudi na kuona chini ya jua…..” ikiwa na maana kuwa ni jambo ambalo amekuwa akiliona mara kwa mara rikijirudia rudia si jambo ambalo linatoke mara moja bali mara nyingi nyingi linatokea duniani. Hata sisi huenda tumewahi kuliona mahali fulani lakini tusijue ama kulitafakari.

Lakini leo tutatazama ni kwa namna gani. Sasa Si wote wenye Maarifa, ufahamu, Ustadi, mbio, Hekima nk, mara zote ndio zinazowasaidia kufanikiwa sana kuliko wale wasiokuwa na vitu hivyo. La!, Ukisoma mwishoni anamalizia na kusema “Lakini wakati wa bahati huwapata wote” unaona hapo!, ikitufundisha pia kuwa majira siku zote habadilika wala hayakai hivyo hivyo milele.

Maana yake ni nini basi ni sawa na leo mtu anaweza akawa na vyeti vya Elimu ya juu sana kama Masters,PHD, nk ikamfanya awe na mafanikio makubwa sana katika maisha yake na nchi kwa ujumla, lakini kuna mwingine ambae hana Elimu kubwa hivyo lakini ana kipawa cha Hekima,ujuzi ama kipaji fulani ambao kazaliwa nao wala hajajifunza kokote kikamfanya apate milango ya mafanikio mingi na akafanikiwa zaidi ya yule mwenye Elimu kubwa.

Hii inatufundisha dhahiri kabisa kuwa Mungu ndie anaetoa na si Mwanadamu kwa utashi wake na nguvu zake. Ukimsoma Yusufu mpaka anakuwa waziri mkuu wa Misri(dunia yote) si kwamba alikuwa na Elimu kubwa sana ya uchumi nk lakini ni Neema tu alipata maana hakustahili kabisa kwanza hakuwa mmsri na pili alikuwa na kesi ya ubakaji halafu anakuwa waziri Mkuu hebu tafakari kwa mwanadamu jambo hili linawezekana??

Lakini yote yako mikononi mwa Bwana. Haleluya!, Mtume Paulo anasema.. Warumi 9:16 “Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu”. Hivyo sisi hatujui pia wakati wetu ni upi!, lakini tendelee kuwa ni wanyeyekevu kwa Bwana yeye atatukweza kwa wakati wake wala tusiwe ni watu wenye kuwadharau wengine wala kuona sisi ndio wateule tumefika tusiwe hivyo kabisa kama wana wa Mungu wakati wako ukifika hata Bwana hataangalia una cheti ama huna umesoma ama hujasoma hivyo endelea kunyeyekea tu kama Neno linavyotwambia.

1Petro 5:6 “Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake”;

Share This Article

Comments

Add Comment
Login to comment Verify your email to comment

No Comments Yet...

There was an error while fetching comments, Please try again later

888888888

mmmmmmmmm

ooooooooo

nnnnnnnnn

ttttttttt

uuuuuuuuu

eeeeeeeee

sssssssss

wwwwwwwww

hhhhhhhhh

rrrrrrrrr

fffffffff

iiiiiiiii

ddddddddd

aaaaaaaaa

yyyyyyyyy

888

mmm

ooo

nnn

ttt

uuu

eee

sss

www

hhh

rrr

fff

iii

888

mmm

ooo

nnn

ttt

uuu

eee

sss

www

hhh

rrr

fff

iii

ddd

aaa

yyy

month

88

88

day

88888

88888

GMT

88

88

hour

:

88

88

minute

:

88

88

second

am

pm

Program Lineup

Previous Article

OUR GREAT COMMISSION
Lets go and cause an Impact.Transformed to Transform.That is great Commission.
2025-06-15 21:00:00
30

Next Article

Faida Ya Kutii Sauti Ya Mungu.
Faida ya kutii sauti ya Mungu maisani mwako,maana ni mwashindi wa hadithi yako,mbona unakata tamaa
2025-07-13 07:00:00
4
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Privacy Policy Terms Of Service
Powered By Caster.fm Streaming Solutions.