error code:
Sounds FM
Sign-In
Verify Email Address Account Sign-Out
Menu
Homepage News
Program
Schedule Shows Specials
Program
Schedule Shows Specials
Staff

Embed The Radio Player In Your Website
Copy the code below and paste it into your website.

Download our desktop apps

Back to news

Unajifunza nini kutokana na Loisi na Eunike

2025-06-20 05:00:00
3
0

 

2 Timotheo 1:1-5 Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu; kwa ajili ya ahadi ya uzima ulio katika Kristo Yesu, kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Neema na iwe kwako, na rehema, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba na kwa Kristo Yesu Bwana wetu.

Namshukuru Mungu, nimwabuduye kwa dhamiri safi tangu zamani za wazee wangu, kama vile nikukumbukavyo wewe daima, katika kuomba kwangu usiku na mchana.

 Nami natamani sana kukuona, nikiyakumbuka machozi yako, ili nijae furaha; nikiikumbuka imani uliyo nayo isiyo na unafiki, ambayo ikikaa kwanza kwa bibi yako Loisi, na katika mama yako Eunike, nami nasadiki wewe nawe unayo.

Hii ni mistari pekee katika biblia ambayo imewatambua Eunike na Loisi kwa majina yao. Loisi ni bibi yake Timotheo na Eunike ni mama wa Timotheo, mistari mingine inawaelezea ila si kwa majina yao. Kwa muda mrefu Timotheo amekuwa msaidizi wa Paulo katika huduma yake.

Paulo aliiona imani kubwa aliyonayo Timotheo na kutambua kuwa imetokana na malezi bora na mafundisho toka kwa mama yake na bibi yake. Aliwatambua wanawake hawa kama watu imara katika imani na katika malezi pia. Matendo 16:1-3 Basi akafika Derbe na Listra, na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke myahudi aliyeamini; lakini baba yake alikuwa Myunani.

Mtu huyo alishuhudiwa vyema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio. Paulo alimtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni myunani. Mama yake Timotheo, Eunike alikuwa ameolewa na mtu wa mataifa na kutokana na kumheshimu mume wake hakimtahiri mtoto wake kama imani yake inavyosema.

Hapa inaonyesha jinsi gani alikuwa mnyenyekevu na mwenye hekima. Pia Eunike alitambua kuwa pamoja na kwamba mtoto wake hakutahiriwa kama ilivyo desturi ya wayahudi, bado yeye analo jukumu la kumfundisha kweli ya Mungu tangu akiwa na umri mdogo.

Alifanya hivi huku alipata ushirikiano toka kwa mama yake Loisi na kwa pamoja walimjengea Timotheo msingi imara wa imani. Matendo 16:2 Mtu huyo alishuhudiwa vyema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio Mistari hii inatuonyesha pia kuwa wanawake hawa hawakusimama peke yao bali walikuwa bega kwa bega na kanisa la Mungu.

Timotheo hakupata mwongozo wa kiroho kutoka kwa baba yake maana hakuwa mwamini lakini mama yake alihakikisha anamuweka karibu kabisa na watumishi wa Mungu, waamini wa mahali pamoja ili waweze kuwa msaada kwake.

Tunajifunza kuwa sisi wanawake tunawajibu mkubwa sana katika kuwafundisha watoto wetu misingi ya neno la Mungu na wokovu. Ni muhimu sana hasa pale ambapo mwenzi wako hajaokoka maana Mungu anakuangalia wewe kuweka misingi bora ya kiMungu ndani ya moyo wa mtoto wako. Usipofanya hivyo shetani atapanda pando lake ambalo itakuwa ni ngumu sana kuling’oa. Ubarikiwe na Bwana Yesu. Share this:

Share This Article

Comments

Add Comment
Login to comment Verify your email to comment

No Comments Yet...

There was an error while fetching comments, Please try again later

888888888

mmmmmmmmm

ooooooooo

nnnnnnnnn

ttttttttt

uuuuuuuuu

eeeeeeeee

sssssssss

wwwwwwwww

hhhhhhhhh

rrrrrrrrr

fffffffff

iiiiiiiii

ddddddddd

aaaaaaaaa

yyyyyyyyy

888

mmm

ooo

nnn

ttt

uuu

eee

sss

www

hhh

rrr

fff

iii

888

mmm

ooo

nnn

ttt

uuu

eee

sss

www

hhh

rrr

fff

iii

ddd

aaa

yyy

month

88

88

day

88888

88888

GMT

88

88

hour

:

88

88

minute

:

88

88

second

am

pm

Program Lineup

Previous Article

OUR GREAT COMMISSION
Lets go and cause an Impact.Transformed to Transform.That is great Commission.
2025-06-15 21:00:00
30

Next Article

Wanawake wa Biblia – Dorcas
Biblia inamwelezea Dorkas kama mwanamke mkarimu sana ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa Yesu.
2025-06-22 07:00:00
5
All Rights Reserved © The Cantona Group PLC||2025
Privacy Policy Terms Of Service
Powered By Caster.fm Streaming Solutions.