WASHAURI WA HAMANI NDIO WALIOMUANGAMIZA HAMANI
Zereshi ( Mke wa Hamani ) na wenye hekima wa Hamani ; Hawa ndio waliomuua na kumwangusha Hamani kwa Ushauri wao; Walimshauri Hamani awaue wayahudi walioko Shushani Ngomeni na wamwandalie Mordekai mti mrefu kwa ajili ya kumnyonga.
(Mordekai alikuwa anasimama kama kiongozi wa kanisa lililokuwa Shushani Ngomeni)
#Esta 5:14 Basi Zereshi mkewe akamwambia, na rafiki zake wote, Na ufanyizwe mti wa mikono hamsini urefu wake, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa kicheko pamoja na mfalme karamuni. Basi neno likampendeza Hamani, akaufanyiza ule mti.
Neno hilo likampendeza Hamani akaufanyiza mti ( Hamani hakuwa anachuja ushauri aliokuwa anapewa ) na wala hakuwa anahesabu gharama ( risk ). Angalia Marafiki hao hao waliomshauri afanye mabaya juu wa watu wa Mungu Israeli , walipoona mambo yamemgeuka wakaongea haya Esta 6:13 [13]Basi Hamani akawasimulia Zereshi mkewe na rafiki zake wote kila neno lililompata.
Kisha watu wake wenye hekima na Zereshi mkewe wakamwambia, Ikiwa huyu Mordekai, ambaye umeanza kuanguka mbele yake, ni wa uzao wa Wayahudi, wewe hutamweza, bali kuanguka utaanguka mbele yake.
Unaona mkewe Hamani anavyomwambia Mume wake ; Anamwambia kuanguka utaanguka mbele ya Mordekai ( mimi nilifikiri watampa mpango wa kumwokoa na kumsaidia ) ; Lakini walimwacha Akafa Esta 7:10 [10]Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia. Mtu mkuu, Mtu aliyewatikisa wayahudi, mtu aliyekuwa na uchu wa madaraka, mtu aliyekuwa anatamani cheo
AKAFA NA MARAFIKI ZAKE HAWAKUONEKANA HAYA MMOJA KUMSAIDIA Washauri wa Hamani ndio waliomuua Hamani
No Comments Yet...